Friday, March 9, 2018

Filamu Yamtaka JB Kupambana na Kitambi


MUIGIZAJI maarufu wa fi lamu Bongo, Jacob Stephen ‘JB’ amefunguka kuwa kupunguza msosi na kufanya mazoezi kumemfanya kuondoa kitambi chake ambacho kilikuwa kikimkera.

Akizungumza na gazeti hili, JB alisema kuwa, kuna fi lamu ambayo walicheza na Single Mtambalike ‘Richie’ na alikuwa akihitajika kufanya mazoezi kwenye fi lamu hiyo na huku alianza kupunguza mlo wake wa kila siku.

“Watu wengi wananishangaa kuwa nimepungua na kitambi nimekikata, lakini kikubwa ni mazoezi ndiyo yamenifanya hivi pamoja na kupunguza mlo. Pia sitaki tena kurudi nilivyokuwa huko nyuma,” alisema JB.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger