Friday, March 16, 2018

Faiza Ally Afunguka, "Sijawahi Kuwaza Kuwa Single Mother"


Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Faiza Ally amefunguka kuwa wakati anakua hakuwahi kuwaza kuja kuwa ‘single mother’.

Faiza ameendelea kufunguka kuwa baada ya kuwa mama akawa anajiuliza ni kwasasababu ya wanaume ndio aishi maisha asiyoyataka? alihoji.
 
Faiza kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika hivi “Wakati nakua sikuwahi kuwaza kuwa single mom, lkn kutokana na misimimo yangu wanaume wajinga hawakunielewa nikajikita ktk kujitegemea, baada kuwa mama nikawa najiuliza ni kwa sababu tu ya mwanaume au baba mtoto ndio niishi maisha nisiyo yataka , nikaondoka nikiwa nauchungu mwingi mno lkn nikasema maisha yangu ni bora kuliko kuwa mke! Nikapitia mengi sana haikua rahisi lkn

 Leo nimesimama imara kwa sababu niliamua kuchagua maisha ninayo ishi kwa hiari ! Nilipita wapi na nikavuka vikwazo vyote ????? Njoo nita share stori yangu na wewe kuwa single mom sio mwisho wako ! Kuna maisha zaidi ya kukaa usipo stahili ! JUA THAMANI YA UANAMKE WAKO BILA KUJALI WANAO BWEKA NJIANI“.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger