Monday, March 5, 2018

Faida zitokanazo na Kucheka Pekee


Bila shaka umewahinkusikia mtu akisema, wach nicheke niongoze siku za kuishi. Kama umewahi kusikia nataka nikuongezee kitu ya kwamba wataalam wa saikolojia wanasema kuwa kucheka au kufurahi ni moja ya tiba kwa afya ambayo huifanya miili yetu kubaki na afya bora zaidi.

Naomba leo nikwambie haya mambo kadhaa ambayo utayapata endapo utakuwa ni mtu wa kucheka na kufurahi.

1. Kwanza kabisa kitendo cha kucheka au kufurahi husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongo wa mawazo na kumfanya mhusika kuwa vizuri kiakili.

2. Husaidia kuimarisha afya ya mapafu
Unapocheka husaidia mapafu yako kutanuka na kuingiza ndani hewa ya safi yaani oxygen. Hivyo unapocheka zaidi tambua kuwa unasaidia kiwango cha hewa kuingia cha kutosha ndani ya mwili na kusaidia damu kusambaa vyema mwilini.

3. Husaidia kuboresha utendaji kazi wa moyo
Kitendo cha kucheka au kufurahi husaidia kukuweka mbali dhidi ya shinikizo la damu la kushuka, kwa sababu husaidia kuongeza mzunguko wa damu mwilini na pia kusaidia mishipa ya damu kutenda kazi vizuri.

4.Huboresha kinga za mwili
Kucheka ni muhimu kwani husaidia kuongeza homoni za hisia ndani ya mwili. Kutokana na mabadiliko hayo huenda.

Hizo ni faida chache kati ya nyingi ambazo mtu akiwa nazo sinamsaidia pia hata kuishi miaka mingi.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger