Monday, March 5, 2018

Fahamu Kilichomuua mchezaji wa Fiorentina


Alizaliwa January 7 mwaka 1987 katika viunga vya San Giovanni Bianco nchini Italia. Davide Astori ni moja kati ya nyota wa mchezo wa Soka aliezaliwa katika mkoa wa Bergamo. Astori alianza kucheza soka la mtaani akiwa mdogo katika timu ya Pontisola na hatimae kipaji chake kikaonekana na haraka akajiunga na shule ya mpira ya watoto ilio chini ya klabu ya AC Milan mwaka 20.

KILICHO MUONDOSHA DAVIDE ASTORI NI HIKI HAPA.
Uongozi wa klabu ya Fiorentina pamoja na wachezaji wapo katika hali ya majonzi na huzuni mara baada ya kumpoteza Nahodha wa klabu yao ya Fiorentina raia wa Italia Davide Astori.

Taarifa zinasema kwamba mlinzi huyo amefariki kutokana na ugonjwa wa ghafla tu, kwa mujibu wa klabu yake. Mchezaji huyo amefariki asubuhi jana ambapo klabu hiyo ikijiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Udinese ambapo baada ya taarifa hizo mchezo huo ukafutwa.

HISTORIA KWENYE SOKA
Astori ambaye aliichezea Italia mara 14, alijiunga na Fiorentina mwaka 2016 akitokea klabu ya Cagliari na kuwachezea mechi 58.

Davide Astori amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 31, Lakini pia ameacha mke mmoja na mtoto wa kike mwenye miaka miwili.

Astori aliwahi kuichezea klabu ya AC Milan katika ujana wake kabla ya kujiunga na Cagliari mwaka 2008. Astori alidumu kwenye shule hio kwa kipindi cha miaka mitano. Mwaka uliofuata Astori alipandishwa timu ya wakubwa ya Milan. Hii ilikuwa ni mwaka 2006.

Bahati mbaya Astoria hakuweza kupata nafasi ya kucheza AC Milan kwani kwa wakati huo palikuwa na walinzi wa kati ambao walikuwa kwenye viwango vya juu kabisa. Astori hakuweza kupenya na kuwaacha kwenye benchi miamba kama Alessandro Costacurta, Kakha Kaladze, Dario Simic, Alessandro Nesta, Daniele Bonera na Nahodha Paolo Maldini.

Hivyo msimu wa mwaka 2008-2009 Astori alihamia klabu ya Cagliari ambao waliingia mkataba wa kummiliki mlinzi Huyo kwa pamoja. Na hatimae Astori akawa chini ya umiliki wa Milan na Cagliari lakini akiichezea Cagliari.

Tarehe 02 mwezi juni mwaka 2011 Cagliari waliamua kununua umiliki uliokuwa chini ya AC Milan na hatimae Davide Astori akawa mchezaji halali wa klabu hio. Tarehe 9 ya mwezi July 2012, Astori aliweka wazi mahaba yake kwa soka la Italia, kwani alikataa  kujiunga na klabu ya Spartak Moscow ya urusi kwa dau lililosemwa la€15 million lililokubaliwa kati ya klabu hizo mbili.

Astori alisema amekataa kuiacha Cagliari ili apate nafasi ya kucheza kwenye timu ya taifa LA Italia. Roma hawakutaka kuendelea na huduma ya Astori hivyo mlinzi huyu akapelekwa kwa mkopo klabuni Fiorentina maarufu kama Viola, klabu inayotoka katika mji was Florence nchini Italia. Hii ilikuwa tarehe 4 August 2015, Astori aliitumikia Viola kwa mkopo hadi Msimu  2017–18 ambapo Viola walimnunua moja kwa moja mlinzi huyu na kumtunuku kitambaa cha nahodha was klabu hio, baada ya aliekuwa nahodha wa klabu hio, Gonzalo Rodríguez kutimka klabuni hapo.

July 24 mwaka 2014, Cagliari walitangaza kuwa mlinzi wao Astori amejiunga kwa mkopo wa mwaka mmoja klabuni Roma.

Mkataba huu uliwapatia Cagliari kitita cha €2m   huku Roma wakiwa na kipengele kwenye mkataba kinacho waruhusu kumnunua moja kwa moja mchezaji huyo endapo watamhitaji na watapaswa kuongeza kiasi cha €5 million. Taarifa ilio tolewa na msemaji wa klabu ya Fiorentina Arturo Mastronardi zilisema kuwa, ilipojiri SAA 3 na nusu Asubuhi ya tarehe 4/3 Astori hakuonekana kwenye rokoo ya chai kwenye kambi ya klabu hio iliopo katika hotel ya LA Di Moret katika viunga vya Friulli mjini Udine, na walipompigia simu zake sambamba na simu ya Hotel hakuweza pokea.

Walipokwenda na kuvunja mlango walimkuta Astori akiwa katika umauti, umauti ambao mpelelezi aliezuru katika tukio hilo bwana Antonio Di Nicolo alisema kuwa ulitokana na maradhi ya ghafla ya moyo. Devide Astori amemuacha mpenzi wake wa muda mreefu bi Francesca Fioretti na kabinti kao ka miaka miwili Vittori.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger