Saturday, March 10, 2018

Dogo Janja Avaa Gauni na Kupaka Lipstiki Kwenye Wimbo wake, Mashabiki wake Wamtolea Mapovu


Stories zilizo-trend kwenye mitandao ya kijamii ambapo msanii wa Bongo Fleva Dogo Janja amewaacha mashabiki wake midomo wazi baada ya kupost picha iliyoacha comments nyingi kwenye ukurasa wake wa instagram.


Dogo Janja amepost cover ya wimbo wake mpya wa Wayu Wayu ambapo ameonekana kuvaa mavazi ya kisichana pamoja na viatu vya kike na pia kupaka lipstick kwenye cover hiyo kitu ambacho ni cha kushangaza kwa jamii za Kiafrika kwa mwanaume kuvaa mavazi ya msichana .

Muonekano huu wa Dogo Janja ambao umezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii ni record ambayo ameiweka katika tasnia ya muziki nchini ambapo hakuna msanii wa kiume ambaye amewahi kufanya kitu kama hicho.


Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger