Thursday, March 15, 2018

Dj Fetty Atoboa Siri Kuhusu Mpango wake Wakurudi Kwenye Utangazaji Hivi Karibuni


September 15 2015 mtangazaji wa zamani wa kituo cha radio cha Clouds FM DJ Fetty alitangaza kuacha kazi ya utangazaji na kuwaaga wafanyakazi wenzake akisema ameamua kupumzika na kuwa atakuwa akifanya biashara zake nyingine.

DJ Fetty alikaa kimya kwa muda mrefu lakini kwa kuwa ni mwanafamilia wa Clouds FM March 8 2017 katika siku ya wanawake duniani alirudi tena XXL na kutangaza katika kipindi maalum kwa ajili ya wanawake duniani na kutangaza tena kwenye XXL.
Kwa mujibu wa post zake mbili za instagram alizozipost usiku wa jana, ya kwanza aliandika “Tizi limeanza. U want me back? weka 👍🏻 zikifika 1000 Mama la mama hewani” lakini baada ya comment 1000 za ndio za kutaka arudi akapost post ni nyingine na kuandika “Pheewwwww 🤐🤐 “1000👍🏻” 🙏🏻🙏🏻 shidddaaaaaah. Now stay tuned for official statement. I love u all” hayo ni maamuzi mazuri kwa Fetty na mashabiki wake.


Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger