Friday, March 16, 2018

Diva Ataja Kiasi cha Pesa Anachotakiwa Kuwa Nacho kama Mahari, Mwanamme wa Kumuoa


Mtangazaji wa Clouds Fm Loveness Malinzi maarufu kama Diva the bawse amefunguka  kuwa hawezi akaolewa na mwanaume yoyote bila  kutokuwa mahari ya shilingi milioni 500.

Hii sio mara ya kwanza kwa Diva kuweka kigezo cha kuolewa na mwanaume mwenye pesa mbele kwani mara nyingi amekuwa akisema kuwa hawezi akaolewa kwa mahari ndogo.

Siku ya jana kupitia ukurasa wake wa Instagram Diva amekumbushia Tena vigezo vikubwa kwa mwanaume ambaye atakubali amuoe ambavyo ni awe tajiri kiasi ya kwamba aweze kutoa mahari ya milioni 500 lakini pia awe anajua kuongea kingereza:

"Kunioa ni milioni 500….set that jokes aside am deadly serious….make sure uwe unaongea English yenyewe hasa… uwe smart uwe handsome…..uwe loaded…No broke niggas in 2018 tupendane kwa faida, you can say wheteves just heard worse, seen worse SMHFG Nothing mean to me…..harsh ain’t new to me I heard it all…..Mwenye povu hana hela ruksa na povu lako nina Omo na jiki plus toothbrush na Colgate jus there for you dummy”.

Diva ametangaza ruksa mwenye hizo sifa ajitokeze hii imekuja baada ya kuachana na mpenzi wake msanii wa Bongo fleva Heri Muziki baada ya kutoswa hewani.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger