Monday, March 12, 2018

DCEA Yamsafisha Wakili Aliyekuwa Akishikiliwa

Kamishna wa Operesheni DCEA, Luteni Kanali Fredrick Milanzi  
Dar es Salaam. Mwanasheria wa kampuni moja ya uwakili ya Law associates, Lizzy Minja ameachiwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) baada ya kujiridhisha hakuhusika kwenye tuhuma za dawa za kulevya zilizokamatwa mwezi uliopita.
Februari 17, Idara ya Uhamiaji iliwakamata watuhumiwa wanane eneo la Masaki wakiwa na dawa za kulevya aina ya cocaine, heroin, bangi na mashine ya kutengenezea dawa za kulevya hizo.
Kamishna wa Operesheni DCEA, Luteni Kanali Fredrick Milanzi alisema kwa sasa wanaoshililiwa ni saba waliohusika na dawa hizo wakiwemo Watanzania wawili.
Wengine raia wa Nigeria ni Bisola Adeyemi, Olasunnanmi Kayode, Aaron Ejeh,Obina Nwauba na Darlinton Nwauba ambaye ni mhitimu wa shahada ya sayansi ya kompyuta kutoka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala tawi la Tanzania.
Kanali Milanzi alisema baada ya kumaliza chuo hicho Nwauba alikuwa anafanya biashara ya dawa za kulevya maeneo mawili anakoishi ikiwemo Masaki na Kijitonyama. “Kati ya Watanzania wawili tuliowakamata mmoja alikuwa rafiki yake wa kimapenzi, mwingine alikuwa wa rafiki ambao wote tumewakamata kwa ajili ya upelelezi zaidi,” alisema Kanali Milanzi.
Naye kamishna wa sheria DCEA, Edwin Kakolaki alisema wanakamilisha uchunguzi wa watuhumiwa saba watapeleka jalada kwa mkurugenzi wa mashtaka(DPP) kwa ajili ya taratibu za kuwapeleka kortini.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger