Thursday, March 15, 2018

BIFU Mpya Mjini, Wasanii Wakufokafoka Watifuana na Kupeana Michambo Kuntu


Wasanii Nikki Mbishi na Moni wa Centrozone wametupiana maneno baada ya hivi karibuni Nikki kusema kuwa kundi jipya la Moni linalofahamika kama MOCO ni lakupita tu wala haliwezi kufika mbali.

 Akiongea kupitia eNEWZ  Moni amesema kwamba  anamshangaa sana Nikki amekuwa ni mtu wa kulalamika na lawama huku akiongeza kuwa siku hizi hata kazi za Nikki  hazioni zaidi anasikika akiwa analalamika tu.

Moni amesema yeye na kundi lake hawafanyi Rap ya kilingeni bali anafanya Rap ya biashara hivyo hayo maneno ya Nikki wala hayamsumbui kwasababu tayari wamefanya kazi nyingi na wanashukuru Watanzania wamewapokea.

Kwa upande mwingine Moni ambaye anatamba na ngoma yake mpya ya Nichum amesema kinachomsumbua Nikki ni uzoefu wake wa kuvunjikiwa na kundi kutokana na uzembe wake huku akimshauri kuwa afanye kazi kwa bidii kwa kuwa anamizizi mizuri na nimuandishi mzuri hivyo asimamie sanaa yake kwanza.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger