Friday, March 9, 2018

Akina Baba Wanaotelekeza Watoto Wao Matatani


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametangaza vita na wanaume wanaowapa ujauzito wanawake na kuwatelekeza kwa kuandaa jopo la Wanasheria watakaoanza kuchukuwa hatua za kisheria kwa wanaume hao kuanzia Aprili 09 mwaka huu kwenye ofisi yake.

Taarifa hiyo imetolea na ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo imesema kwamba kitendo cha Wanaume kukwepa majukumu ya malezi na matunzo kwa mtoto imepelekea pia baadhi yao kutoa ujauzito, kutupa watoto na wengine kupeleka wajukuu kulelewa na wazee na kusababisha mzigo kwa familia.

Aidha RC Makonda amesema kuwa wataangalia pia utaratibu wa kufanya marekebisho sheria ya gharama za matunzo ya mtoto kwakuwa ni ndogo na haiendani na hali ya sasa.

RC Makonda amesema lengo lake ni kuleta ukombozi kwa kinamama ili kuhakikisha wakihitaji fedha ya matumizi wanapatiwa na sio kupigwa, kusimangwa, kutukanwa na kudhalilishwa.

Hata hivyo Makonda amesema katika zoezi hilo lengo lake ni kuleta ukombozi kwa kinamama ili kuhakikisha wakihitaji fedha ya matumizi wanapatiwa na sio kupigwa, kusimangwa, kutukanwa na kudhalilishwa.

Pamoja na hayo Kiongozi huyo wa Mkoa wa Dar es salaam amesena kwamba  ameamua kutoa muda wa mwezi mmoja ili kama kuna baba kwenye huu Mkoa huo anajijua ametelekeza mtoto na hatoi fedha za matunzo akamtafute na kuanza kutoa matunzo kwakuwa itakapofika Aprili 09  atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger