Friday, March 9, 2018

Ajali Yasababisha Vifo vya Watu 4 Mbeya


MBEYA: Watu wanne wamefariki dunia na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Super Rojas kugongana na lori jana Machi 8, 2018 katika eneo la Igawa wilayani ya Mbarali mkoani Mbeya.

Ajali hiyo imetokea katika barabara inayounganisha mikoa ya Mbeya na Iringa, baada ya basi hilo lenye namba za usajili T 170 DKS lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Njombe kugongana na lori lenye namba za usajili T 838 DRE aina ya Scania lililokuwa limebeba kontena.


Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger