Saturday, March 10, 2018

Ahukumiwa Miaka 50 Jela Kwa Kumuua Mtoto Wake Akiwa Anamtoa Mapepo


Mwanaume mmoja nchini Ujerumani mwenye umri wa miaka 5o amehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela baada ya kumuua binti yake aliyekuwa na matatizo ya akili kwa kumkanyaga hadi kufa.

Inaelezwa kuwa kutokana na matatizo ya akili ya binti huyo, baba huyo aliamini kuwa mwanaye ana mapepo hivyo kuamua amuombee kwa kumkanyaga ili yamtoke jambo lililosababisha binti huyo kupoteza maisha.

Mwanaume huyo pia alishutumiwa kujihusisha kimapenzi na mtoto wake huyo ambaye hakuwa sawa kiakili, pia akiamini itasaidia kumponya ‘mapepo’ hayo.

Kwenye kusikilizwa kesi hiyo, ilioneshwa video ambayo ilionesha baba huyo amesimama juu ya mwili wa mwanaye huyo wa miaka 26, akimkanyaga tumboni hadi binti huyo kufariki.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger