Sunday, February 18, 2018

Watu 66 wafariki kwenye ajali ya ndege


Watu 66 wamefariki papo hapo kwenye ajali mbaya ya Ndege iliyotokea leo asubuhi huko nchini Iran baada ya kuanguka mlimani.

Ndege hiyo yenye namba ATR-72 iliyokuwa ikisafiri kutoka Tehran kwenda jijini Yasuj imedondoka katika milima ya Semirom iliyopo kusini mwa Iran.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la habari la AP, Watu wote waliokuwemo kwenye ndege hiyo wamefariki huku chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger