Thursday, February 22, 2018

VIDEO: Familia ya Aquilina Yaishukuru Serikali kwa Kuridhia Kugharamia Mazishi ya Mtoto Wao


Dar es Salaam. Familia ya marehemu  Akwilina Akwiline inaendelea na maandalizi ya mazishi, huku ikielezwa kuwa Serikali imekubali kuyagharimia lakini si kutoa fedha.

Serikali imefikia hatua hiyo baada ya jana Februari 20,2018 familia ya Akwilina kueleza kuwa bajeti ya mazishi ni Sh80 milioni.

Katibu wa kamati ya mazishi Moi Kiyeyeu, ambaye ni kaka wa Akwilina amesema Serikali imewajibu kuwa haitawapa fedha taslim bali itagharimia vitu vilioorodheshwa katika bajeti ya mazishi hayo.

"Tulipotoa bajeti hatukuwa na maana kuishinikiza Serikali itoe fedha zote bali ilikuwa mahitaji ya msiba hadi pale utakapoisha. Tunashukuru Mungu kwa Serikali kuridhia kugharimia," amesema Kiyeyeu.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger