Sunday, February 18, 2018

TDC watoa msaada kwa Manusura Luck Vincent


Umoja wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi Tanzania Global Diaspora Council (TDC), umekabidhi Sh3 milioni kwa waliokuwa wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent walionusurika katika ajali.

Fedha hizo zilikabidhiwa na mjumbe wa TDC anayeishi Kampala Uganda, Grace Kijuu kwa wazazi wa wanafunzi katika hafla fupi iliyofanyika jijini Arusha.

Waliokabidhiwa Sh1 milioni kila mmoja ni Grace Elibariki, mzazi wa mwanafunzi Doreen Mshana, Zaitun Ismael ambaye ni mzazi wa Saidia Ismael na Mwema Francis, mzazi wa Wilson Tarimo.

Katika ajali iliyotokea Mei,2017 eneo la Rhotia Marera huko Karatu, wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja walipoteza maisha baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka.

Akikabidhi fedha hizo, Kijuu amesema baada ya ajali hiyo, Watanzania waishio na kufanya kazi nje ya nchi waliamua kuwachangia manusura wa ajali hiyo.

Kukabidhiwa kwa fedha hizo kunatokana na taarifa iliyochapwa na gazeti hili Januari 15, 2017  ikiwanukuu baadhi ya wanajumuiya wakilalamika kutokabidhiwa kwa fedha hizo tangu wazichange.

Baada ya kuandika kwa taarifa hiyo, kiongozi wa jumuiya hiyo aliyekuwa amezihodhi fedha hizo, alimteua mwandishi mmoja wa habari wa Tanzania ili amtumie fedha hizo akazikabidhi.

Hata hivyo, kulitokea mvutano wa kiwango halisi kilichochangwa huku kiongozi huyo akidai ni Sh1.75 milioni, lakini wajumbe wakadai kumbukumbu zao zinaonyesha walichanga Sh2.4 milioni.

Katibu wa TDC anayeishi Australia, Dk Casta Tungaraza alipoulizwa juu ya tuhuma zinazomkabili mmoja wa viongozi wao, hakuthibitisha wala kukanusha.

“Sina maelezo reliable (ya kuaminika) kuhusu hizo allegation (tuhuma),” alijibu kwa kifupi alipoulizwa hatua ambazo wameshazichukua kukabiliana na mgogoro huo ulioibuka.

Mvutano huo ulisabababisha kiongozi huyo kukubali kujazia kiwango ambacho kimepungua na fedha zilizokabidhiwa kufikia Sh3 milioni siyo Sh1.75 zilizokuwa zikabidhiwe awali.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger