Wednesday, February 28, 2018

Mtoto wa Miezi Minne Aibiwa Kanisani…ilikuwaje?


Jeshi la Polisi nchini Kenya linamshikilia Binti wa miaka 22 kwa tuhuma za kuhusishwa na wizi wa mtoto wa umri wa miezi minne wakati wako ndani ya kanisa katika Jimbo la Kirinyaga nchini humo.

Inaelezwa kuwa binti huyo alikutwa na mtoto huyo aliyepotea tangu Jumapili ya February 25, 2018 katika kanisa la Jesus Winner lililopo katika kata ya Mitheru. Binti huyo amekutwa na mtoto huyo katika Jimbo jingine la Nithi.

Kwa mujibu wa mama wa mtoto Fidelis Mugo, alimwacha mwanae amebebwa na rafiki yake alipoenda kushughulikia jambo nje ya kanisa na pindi aliporudi rafiki aliyeachiwa mtoto alisema kuwa kuna muumini mwingine wa kanisa hilo aliomba ambebe.

Muumini huyo alitafutwa kanisani hapo lakini hakupatikana na ndipo ikabidi taarifa itolewe polisi na jitihada za kumtafuta mwizi wa mtoto huyo zilipoanza kufanyika.
   

   


   
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger