Tuesday, February 27, 2018

Mbowe Amuwashia Moto Msajili "Mtungi Ndio Mtu Pekee Anayeharibu na Kuvuruga Vyama Siasa"


Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe amefunguka na kudai Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mtungi ndio mtu pekee anayeharibu na kuvuruga vyama siasa kuliko kiongozi mwingine yeyote yule aliyewahi kutokea.


Mbowe amebainisha hayo leo (Februari 27, 2018) wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari katika makao makuu  ya CHADEMA eneo la Magomeni, jijini Dar es Salaam baada ya kupita siku kadhaa tokea Jaji Mtungi kuipa barua chama hicho cha siasa kukitishia kutaka kukifuta.

"Muda unavyozidi kwenda namtambua vizuri Jaj Mtungi ni mtu wa aina gani. huyu ndio mtu anayevuruga vyama vya siasa kuliko kiongozi mwingine yeyote yule katika majaji au wasajili waliokwisha kutangulia tangu tulipo anzisha vyama vingi", amesema Mbowe.

Pamoja na hayo, Mbowe ameendelea kwa kusema 'lakini niseme tu ndugu zangu hizi chaguzi zote zitaendelea kuzaa majeraha na maumivu, kama hatuwa 'serious' hazitachukuliwa na kama 'movement serious' haitochukuliwa katika nchi hii kwa sababu hawa wenzetu hawaoni aibu wanajipanga na kulindwa na dola".

Kwa upande mwingine, Mbowe amesema chama cha CHADEMA sio chama cha kigaidi kama wanavyodhania bali ni chama makini kilichokuwa na mkusanyiko wa makabila na dini zote.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger