Thursday, February 15, 2018

Mange Kimambi Azishukia Biashara za Network Marketing na Bahati Nasibu Bongo


Mange Kimambi Azishukia Biashara za Network Marketing na Bahati Nasibu Bongo


Ameandika haya:

Samahanini nimewasahau AIM na Trevo kwenye listi hapo.
.
Hao Q-net, Global Alliance etc, hizo ndo ponzi scheme ambazo ni illegal. Kwa Tz it seems hizi kampuni huwa zinafanya kazi na viongozi wa serikali sababu huwa wanaachwa walize watu wengiii alafu ndo serikali inajitia kuingilia kati. Mnakumbuka Deci, Telex Free, D9, zote zilikufa na kuliza watu, alafu ukute ndo wale wale Ila wanakuja na majina tofauti 😂.As you can see Waziri .... aliwajengea Qnet uaminifu mkubwa kwa wananchi ili awawezeshe kutapeli watu.

Sio kila anaeingia kwenye hii Qnet, Global au Aim anatapeliwa, wale walioingia mwanzo kabisa kampuni ilipoanza tena huwa ni wachache mnooo wale kweli wanatapa faida. Ila wengine woooote wa baadae wanatapeliwa.

Ukiacha hao matapeli wa wazi wazi kama Qnet na AIM kuna hizi kampuni kubwa wao wanafanya utapeli kwa njia halali na kampuni hizo ni kama forever Living, Oriflame, Trevo.Zote hizi ni prymid schemes. Ni mwaka jana tu Advertising Standards Bureau ya UK iliwaanika Forever living kwa kusema uwongo kuhusu manufaa ya products zao na kwamba hizo products hazina benefits hizo wanazozitangaza.Forever living, Oriflame ni upupu ukishaingia wewe pressure kubwa ni kuingiza wauzaji wengine na kila mtu anajiunga kwa kutoa fedha.msijione wajinga peke yenu hii hata wazungu wameumizwa,kinachosikitisha sana ni kwamba kuna wagonjwa wanaacha dawa na kutumia products hizi wakiamini zitawasaidia na hakuna cha kupungua weight wala nini. Alafu unaweza piga kazi kama punda ukakuta kwa mwezi umeingiza elfu 50, profit kubwa wanapata wale waliojuu kabisa ya pyramid kila wewe unapouzia watu bidhaa feki ambazo benefit zake zimeshapingwa.

Hao Biko sijui 3 mzuka hizo ni bahati nasibu ambazo zipo nchi nyingi tu hata hapa marekani zipo. So inawezekana hata za TZ ni za kweli ila tatizo ni moja tu hii industry ya bahati nasibu kwa Tanzania haijawa regulated vizuri kwa hiyo kuna mwanya mkubwa sana wa matapeli kuendesha hizi lottery. Wanaweza tu kupozisha ndugu zao au mahouseboy wao kuwa wameshinda mamilioni kumbe hakuna anaeshinda. hilo ndo tatizo naloliona hapa.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger