Tuesday, February 27, 2018

Hizi Ndio Kanuni Za Kuishi Maisha Marefu


Je wewe ni miongoni mwa watu ambao wanapenda kuishi miaka mingi kama mimi, kama jibu ni ndiyo basi siri ya kuweza kusihi maisha marefu ipo katika Makala haya. Si uchawi bali ni kutokana na wataalamu wa moyo limeelezea masuala muhimu ambayo yanamsaidia mtu kuishi maisha marefu kama ifuatayo:-

Uchunguzi huo umeonyesha kwamba watu wengi umri wa kuanzia miaka 50 ambao wanaishi kwa kufuata masharti hayo huwa na uwezo wa kuishi miaka 40 zaidi bila kupata shinikizo la damu na ugonjwa wa moyo, ambayo ni magonjwa makuu mawili yanayoua watu zaidi duniani.

Wataalamu wamesema kwamba, kila mtu anayetaka kuishia maisha marefu anatakiwa kufuata ushauri ufuatao:


Jiepushe kuvuta sigara au acha kuvuta sigara kabisa.
Hakikisha BMI yako haizidi 25.
Kila wiki pata dakika zisizopungua 150 za kufanya mazoezi ya kawaida.
Jitahidi kufuata maelekezo ya kula lishe bora ambayo ni: vikombe 4 na nusu vya matunda na mboga mboga kwa siku, samaki mara mbili au tatu kwa wiki. Usinywe sana vinywaji vyenye sukari, kula vyakula vyenye ufumwele kila siku na chumvi isizidi miligram 1,500 kwa siku.
Kiwango cha kolestero au mafuta katika damu yako kisizidi 200.
Shinikizo lako la damu lisiwe zaidi ya 120 chini ya 80.
Sukari katika damu iwe chini ya 100.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger