Thursday, February 22, 2018

Godbless Lema: Nawatakia Kila la Heri Madiwani Waliohama na Kujiunga na CCM


Ninawatakia kila la kheri Madiwani waliojiunga na CCM leo katika nchi yenye mfumo wa siasa za vyama vingi uamuzi kama huu unaweza kuwa sawa kama utashi wa maamuzi haya ungewezwa kujengwa katika maadili na ukweli.

Safari hii ya mageuzi ya kujenga demokrasia ni safari ngumu sana wengi wameamua kuuza haki na utu wao na wengine wataendelea, bila shaka ni dhahiri kuwa Taifa letu linapita katika changamoto nyingi kwa sasa kushambuliwa kwa demokrasia kwa njia yoyote Ile sio hasara ya CHADEMA bali ni hasara ya nchi yetu.

Kwa mtu mwenye akili timamu hata ndani ya CCM huwezi kuruhusu kuuawa kwa demokrasi ya Nchi kwa sababu tu ya faida mfu ya chama chako madhara makubwa kichama hayako kwetu bali zaidi yatakuja kuonekana huko CCM kwani hatuna muda mrefu biashara kama hii italeta shida ndani kubwa ndani yao na chama tawala kinapokosa busara ya kutawala sio faida kwa upinzani bali ni hasara kwa Taifa.

Hata hivyo nafikiri tuko kwenye wakati mzuri sana wa mageuzi ya nchi yetu tunapaswa kujipa muda kidogo, haikuwa kazi rahisi Israel kutoka Misri na na kufika Kanaani lakini walifika.

Nchi hii itafikia kilele muhimu cha haki mara nyingi mambo mengi katika Dunia yana amuliwa na muda, tafadhali msiwaze chuki dhidi yao kwani watu wa hii wanaendelea kuwa msaada wa utafiti kwetu wa fikra ndani ya nchi yetu nakufanya tathimini ya kweli ya safari hii muhimu ambayo sijui tutafika lini lakini lazima kuwepo kwenye lengo bila kuyumba ili uhuru wetu uonekane kesho.

Arusha MSIOGOPE.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger