Thursday, February 22, 2018

CHADEMA Watoa Tamko Kuhusu Watu 40 Waliokamatwa Siku ya Maandamano


Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kitalishtaki Jeshi la Polisi na Serikali endapo watashindwa kutoa tamko kuhusu watu 40 waliokamatwa siku ya maandamano katika uchaguzi mdogo wa ubunge Kinondoni.

Akizungumza jana  na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika alisema watu hao 40 walikamatwa February 16, 2018 wakati wakielekea Manispaa ya Kinondoni na miongoni mwao walikuwa ni wapita njia tu na wengine ni watoto waliochini ya miaka 18.

Mnyika alisema hadi sasa Jeshi la Polisi linawashikilia wananchi hao 40, ambapo kisheria lilipaswa kutoa haki kwa wananchi hao kupata dhamana.

“Tunalitaka jeshi la Polisi kupitia IGP kutoa kauli  juu ya watu hao 40 wanaowashikilia na kuwaainisha kwa majina watu hao na kueleza taratibu za kuwapa dhamana ama iwapeleke Mahakamani.”  Alisema John MnyikaShare:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger