Monday, February 19, 2018

CHADEMA “Mwigulu, Masauni na IGP Sirro wanasubiri nini ofisni”


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani Dr. Mwigulu Nchemba, Naibu wake  Engineer Masauni pamoja na IGP Simon Sirro wajiuzulu kufuatia kifo cha Mwanafunzi wa NIT, Akwilina.

Akiongea na Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amesema muendelezo wa matukio haya ikiwemo la mwanafunzi ni utamaduni mpya katika siasa ambao ni muendelezo wa kushambuliwa kwa watu mbalimbali akiwemo Tundu Lissu.

Pia CHADEMA kimelitaka Jeshi la Polisi wamhoji Humphrey Polepole kutokana na tuhuma alizozitoa dhidi ya Chama hicho kwamba walikusanya kundi la vijana akiwemo huyo mwanafunzi kwa ajili ya kuandamana.

“Tunalaani na tunasikitishwa na mauaji yaliyofanywa kwa mwanafunzi huyu, kwani huu ni muendelezo wa matukio ya mauaji na kuteka watu,”-Mrema

“Tunamtaka Masauni na Mwigulu wakumbuke Mwinyi alijiuzulu wakati wafungwa walipofia Gerezani Shinyanga, IGP anafanya nini Ofisini, Mwigulu anafanya nini ofisini, hivyo tunataka waachie Ofisi,” -Mrema.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger