Wednesday, February 28, 2018

Baada ya Tetesi Chirwa Anakwenda Simba, Yanga Yajibu Mapigo


Tayari tetesi zimeanza kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kwamba, mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa huenda akajiunga na ‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba mara baada ya kumaliza mkataba wake na yanga ambao kwa sasa unaelekea ukingoni.

Mwenyekiti wa usajili na mashindano Hussein Nyika amekanusha tetesi hizo kwamba si za kweli huku akisisitiza Chirwa haendi popote labda kama Yanga wataamua kuwachi lakini si vinginevyo.

“Hawezi kwenda sehemu yoyote isipokuwa hadi sisi tutakaposema nenda lakini kama bado tunamuhitaji, hawezi kwenda sehemu yeyote”-amesema Hussein Nyika ambaye ni mwenyekiti wa usajili ndani ya Yanga.

“Niwatoe wasiwasi wapenzi na wanachama wa Yanga kwamba, mchezaji ambaye yupo Yanga si dhani kama anaweza kuondoka kwenda sehemu yoyote labda hadi Yanga watakapoamua aondoke lakini kama bado wanamuhita
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger