Wednesday, December 20, 2017

Wakili Albert Msando na Zitto Kabwe Wajibizana Kuhusu Mafao ya Wastaafu Kukatwa Kodi

Zitto Kabwe: Sio Rahisi Ujue au Uelewe Kila Kitu.

Nimesoma alichoandika Ndugu yangu Zitto Kabwe (MB) akisema kwamba kifungu cha 47(3) cha Public Service Social Security Fund Act, 2017 kinaelekeza kwamba mstaafu akatwe kodi kwenye pensheni yake. Huu ni UPOTOSHAJI.

Ni vyema masuala ya tafsiri ya sheria yakaachwa kwa wataalamu wa sheria wa chama chake. Ni wazi kabisa wakati anaandika hakuwa amewauliza wanasheria kwenye chama chake wamsaidie tafsiri sahihi ya kifungu hicho.

Kwa akili za kawaida utaona kabisa ndugu yangu Zitto anajaribu kupotosha kwa kuamini kwamba wafanyakazi wa umma ni mtaji wa kisiasa na kuwasemea anapata uhalali wa kuwa 'kiongozi anayewajali'.

Tukisome kwa pamoja kifungu hicho;

(3) A pension, gratuity or any allowance granted under this Act, shall not be attached, sequestered or levied upon for or in respect of any debt, mortgage or claim other than a claim of income tax due to the Government but, the Director General shall make arrangement necessary for satisfying it or any debt arising from, discharging a mortgage created or an order of the court issued consequent upon a loan granted to a member.

Kifungu hiki hakielekezi makato ya income tax. It is not a charging section!! Kifungu hi ho kinasema kwamba 'a pension, gratuity or any allowance' SHALL NOT be attached, sequestered or levied upon...unless it is a CLAIM OF INCOME TAX. Yaani kama kuna 'madai ya income tax'. Endapo mstaafu anadaiwa income tax basi pension, gratuity or any allowance may be attached, sequestered or levied upon. It is that basic and elementary!!

Sidhani kama Ndugu yangu Zitto anataka kuuambia umma kwamba mstaafu kama anadaiwa income tax mafao yake yasiwe attached!! Kwa hiyo asilipe!??

Vile vile Ndugu yangu Zitto ni mjumbe wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii. Je ameshiriki mijadala kwenye Kamati yake? Hiyo tafsiri yake ya kifungu hicho aliijadili huko kwenye Kamati? Alijibiwa nini? Ingekuwa amefanya hivyo asingejikuta katika kutokuelewa huku.

Tubaki kwenye 'constructive criticism' kusaidia kuwa na sheria bora ambayo italinda maslahi ya wafanyakazi wa umma. Bado kuna nafasi ya kuwatetea na 'kuonekana' unawatetea bila kupotosha tafsiri ya sheria.

#KunaMudaWaKukaaKimya #UkimyaNiBusaraPia

By Alberto Msando - Dodoma Tanzania.
MAJIBU YA ZITTO KABWE KWA MSANDO​

Hoja ya Albert Msando na majibu yangu kuhusu Muswada wa Sheria mpya ya Pensheni

Nimeambiwa kuwa Mdogo wangu Msando Alberto kaandika haya. Sina hakika kama ni yeye lakini nitajibu.

Kaandika

Zitto Kabwe: Sio Rahisi Ujue au Uelewe Kila Kitu.

Nimesoma alichoandika Ndugu yangu Zitto Kabwe (MB) akisema kwamba kifungu cha 47(3) cha Public Service Social Security Fund Act, 2017 kinaelekeza kwamba mstaafu akatwe kodi kwenye pensheni yake. Huu ni UPOTOSHAJI.

Ni vyema masuala ya tafsiri ya sheria yakaachwa kwa wataalamu wa sheria wa chama chake. Ni wazi kabisa wakati anaandika hakuwa amewauliza wanasheria kwenye chama chake wamsaidie tafsiri sahihi ya kifungu hicho.

Kwa akili za kawaida utaona kabisa ndugu yangu Zitto anajaribu kupotosha kwa kuamini kwamba wafanyakazi wa umma ni mtaji wa kisiasa na kuwasemea anapata uhalali wa kuwa 'kiongozi anayewajali'.

Tukisome kwa pamoja kifungu hicho;
(3) A pension, gratuity or any allowance granted under this Act, shall not be attached, sequestered or levied upon for or in respect of any debt, mortgage or claim other than a claim of income tax due to the Government but, the Director General shall make arrangement necessary for satisfying it or any debt arising from, discharging a mortgage created or an order of the court issued consequent upon a loan granted to a member.

Kifungu hiki hakielekezi makato ya income tax. It is not a charging section!! Kifungu hi ho kinasema kwamba 'a pension, gratuity or any allowance' SHALL NOT be attached, sequestered or levied upon...unless it is a CLAIM OF INCOME TAX. Yaani kama kuna 'madai ya income tax'. Endapo mstaafu anadaiwa income tax basi pension, gratuity or any allowance may be attached, sequestered or levied upon. It is that basic and elementary!!

Akauliza

SWALI: Sidhani kama Ndugu yangu Zitto anataka kuuambia umma kwamba mstaafu kama anadaiwa income tax mafao yake yasiwe attached!! Kwa hiyo asilipe!??

Nimemjibu

JIBU: tuanze na claim of income tax. Mtumishi claim yake ya income tax ni nini? Sio PAYE? PAYE Mfanyakazi atadaiwa wakati inakatwa moja kwa moja kwenye mshahara? Mtumishi wa Umma hawezi kudaiwa kodi ya mapato kwa sababu inakatwa na Mwajiri moja kwa moja. Siamini kama mdogo wangu Albert Msando anaweza kuwa na hoja nyepesi namna hii. Albert ninayemjua ana uwezo mkubwa kuona hili. Nina mashaka kuwa ukiwa CCM nusu ya akili inaondoka kichwani.

Akauliza tena

SWALI: Vile vile Ndugu yangu Zitto ni mjumbe wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii. Je ameshiriki mijadala kwenye Kamati yake? Hiyo tafsiri yake ya kifungu hicho aliijadili huko kwenye Kamati? Alijibiwa nini? Ingekuwa amefanya hivyo asingejikuta katika kutokuelewa huku.

Nikamjibu

JIBU: Kuhusu Kamati huyu mwandishi ni hajui taratibu za Bunge na siamini huyu kuwa ni Albert. Kwanza muswada huu unakwenda Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya kina Ally Saleh Mwenyekiti Mchengerwa. kwa sababu ndio inahusika na social security. Kamati ya Huduma za Jamii ambayo mimi ni mjumbe haihusiki na muswada huo. Kamati za Bunge zinaanza kazi katikati ya January 2018. Sasa mtu anaposema nimefanya nini ni wazi hajui kazi za Bunge wala ratiba za Bunge. Sasa nashiriki vipi kazi za mwaka kesho?

Akasema

HOJA: Tubaki kwenye 'constructive criticism' kusaidia kuwa na sheria bora ambayo italinda maslahi ya wafanyakazi wa umma. Bado kuna nafasi ya kuwatetea na 'kuonekana' unawatetea bila kupotosha tafsiri ya sheria.

Nikafafanua

JIBU: ndugu yangu naomba Niambie kifungu kwenye sheria mpya ambacho kinatoa exemption ya kodi kwenye pensheni. Sheria inayotumika sasa ipo wazi sana kifungu cha 7. Nionyeshwe kifungu kama hicho kwenye sheria inayopendekezwa.

Nasaha zangu kwa ndugu yangu wa damu

Ni kweli kabisa #KunaMudaWaKukaaKimya #UkimyaNiBusaraPia kama asemavyo ndugu yangu Msando. Namshauri ndugu yangu akae kimya aache sisi tunaotetea wanyonge tuendelee kuwatetea. Yeye akae kimya tunamwelewa.

Zitto Kabwe, Dar es Salaam.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger