Tuesday, December 19, 2017

Vituko vya Mpenzi Wangu wa Sasa Vimenifanya Nimkumbuke Huyu Binti

Siku za ujana zinaenda kasi sana nagundua kuna mambo kadhaa niliyaacha kwa kutoona thamani yake ila kwa sasa nagundua kuwa ilikuwa bahati ambayo sikuweza kuing'amua kwa zama zile.

Nimepata Frustration za kutosha katika mahusiano nashukuru Jamii forum inanipa nguvu sana kupambana na hali yangu, Kipindi fulani nikiwa nipo masomoni Nilipata kujuana na dada mmoja eneo lile ambalo nilikuwa naishi, Queen Jina ambalo alikuwa akilitumia kwenye Mtandao wa Facebook. Mimi na Queen tulikutana Facebook na ikatokea mawasiliano kati yangu na yeye na hatimaye chembechembe za mahusiano zikaanza siku chache baada ya kujuana, Niliangalia Profile yake nikagundua yupo karibu sana na eneo langu ikabidi jioni moja niombe kukutana nae, Kweli Queen alikubali na kwa mara ya kwanza nilienda kuonana nae nakumbuka ilikuwa jioni na hali ya hewa ya ubaridi ya Arusha ilikuwa imetanda kwenye kila kona ya Mji.

Hatimaye nilionana na Queen na tukajuana kwa sura acha awali tulipojuana kwa picha, Hakika naandika haya nikiwa namkumbuka huyu dada maana huyu Pasua kichwa wangu ananifanya nijilaumu kwanini niliacha "Mbachao kwa msaala upitao" Tulitumia dakika chini ya 10 kwenye maongezi yetu, nakumbuka aliniuliza umekula nikamjibu sina kasumba ya kupika usiku endapo mchana nimekula hivyo sitahitaji kula kwa usiku, aliona huruma sana kwani nilikuwa nimepanga najua mnafahamu maisha ya wanaume hasa wakiwa wamepanga wengi uvivu wetu ni kupika, Basi Quuen aliomba twende sehemu aninunulie chakula tule pamoja kisha tuagane ila nilikataa kwa kumtaka asiwe na shaka hata kidogo mimi niko sawa Mwisho kabisa alidai nimsubiri kidogo aliondoka na kurudi baada ya Dakika kadhaa huku akionekana kama hana furaha, nikamuuliza mbona umenyong'onyea akadai hapana nilienda kukutafutia chapati uende nazo ila nimekosa itabidi uende na Hiki kinywaji ila moyo wangu ungekuwa na furaha kama ungeenda na chakula Ukale. Alinipa Red Bull ambayo alikuja nayo na nikaagana nae na kurudi kunako makazi yangu.

Nilipofika nilimpa taarifa kuwa tayari nipo kwenye makazi yangu na tukaagana kwa kutakiana usiku mwema kisha nikanywa kile kinywaji nikalala hadi asubuhi nilipoamka na kukuta ujumbe wake ukiniamsha, Kiukweli ulikuwa ni muda mfupi toka tujuane nae ila Quuen alionekana wazi kuwa anahitaji mahusiano ambayo yangemfanya awe na furaha kuna mambo hayakuwa sawa kwa upande wake (Mambo ya Kifamilia).

Jioni aliniomba tukutane tena na nilienda nikaonana nae, Queen alikuwa ni mhitimu wa taaluma ya ualimu ngazi ya cheti na alitaka kurudi chuo kujiendeleza, Nilipofika aliniambia dukuduku lake kuwa katika familia yake analazimishwa kuolewa na mtu ambaye yeye hampendi kwa sababu yule jamaa anawasiliana na wazazi wake badala ya kuwasiliana na Binti mwenyewe hivyo wazazi wakampa uhuru kwa yule binti bila ya ridhaa yake. Quuen aliongeza kuwa anapenda apate mtu ambaye moyo wake ungefurahia kuwa nae hata kama hana mali ila awe na mapenzi ya dhati kwake, kiukweli kipindi kile nilikuwa bado sijawaza kama naweza kumpenda mtu maana nilikuwa nawaza mambo mengine sio mahusiano.


Basi siku ile ya pili alikuwa na furaha kuliko jana yake tulivyoonana kwa mara ya kwanza na ilibidi hata kukubali kupata busu na mambo mengine yenye kuonesha kuwa naweza kuwa Shujaa wake kwenye mahusiano, Kumbe mimi sikuwa nimeweka mawazo sana kwake kama yeye alivyokuwa ameweka mawazo kwangu. Siku ya 3 alitaka niende kwao na nilienda na kuonana na wadogo zake na kutambulishana pale kwa muda kisha tukatoka kwenda sehemu maalum kwa ajili ya maongezi, hakika mwanamke mchafu tabia hujulikana hata kwa macho ila kwa Quuen ni kama niliokota boksi la Chawa na kuacha boksi la senene ki ukweli wanasema wanawake wenye tabia nzuri ni wa kutafuta hakika nimeamini baada ya kupasuliwa kichwa na huyu Vuvuzela kiukweli jana nilijikuta naanza kumtafuta Queen hata niombe tu msamaha ili nione kama ile kampeni yetu ya mwanzo ingeweza kuendelea ila kadri ya uwezo wangu juhudi ziligonga mwamba.

Yeye alikuwa anafanya kazi kwenye salon moja ya kike hadi natoka Arusha na kwenda huko kwingineko nilishindwa hata kuaga hapo ndipo aliona sina muda na yeye na hata alipogundua kuwa nimeondoka Arusha aliniambia sawa nakutakia maisha mema dah! Hadi leo kweli naona nimetakiwa maisha mema.


Mungu awabariki wanawake wote ambao wapo kama Quuen alikuwa ni mwanamke wa kuao kabisa "Golden Chance never come Twice", huwenda nayapata yote haya kwa sababu nilishindwa kuchagua sehemu sahihi

By Raphael wa Ureno
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger