Tuesday, December 19, 2017

Shein kuzindua kongamano la Kiswahili mjini Unguja leoTaarifa iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (Bakiza), Mohamed Seif Khatib inaeleza kuwa kongamano hilo la siku mbili litajadili mada 100 zitakazowasilishwa na wageni, zikiwamo makala maalumu zinazohusiana na lugha hiyo.

“Kwenye mada 100 ndani yake kuna makala zitakazokuwa na mchango mkubwa katika kuikuza lugha ya Kiswahili kwa masilahi ya vizazi vya sasa na vijavyo,” alisema Khatib.

Alibainisha kuwa zaidi ya washiriki 100 wanatarajiwa kushiriki kongamano hilo wakiwamo wataalamu wa Kiswahili wa ndani na nje ya nchi, taasisi za kiraia, wataalam na wanafunzi kutoka vyuo vikuu pamoja na wananchi.

Katibu mtendaji wa baraza hilo, Mwanahija Ali Juma aliwataka wananchi kuchangamkia fursa ya kongamano hilo kwa kushiriki ili nao waweze kuongeza utaalamu zaidi katika kutumia misamiati ya lugha yao.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger