Monday, December 18, 2017

Rais Magufuli ; CCM Kimekuwa Chama Imara na Kinaendelea Kuwavutia Watu


Leo Mwenyekiti wa Chama cha  Mapinduzi taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema CCM kimekuwa chama imara na chama kinachoendelea kuwavutia watu wengi kila siku ikiwemo viongozi na wanachama kutoka vyama upinzani nchini.

Rais Magufuli amesema kuwa kutokana na uimara wa CCM amepokea majina nane ya madiwani wa vyama vya upinzani na Mbunge mmoja ambapo wanasubiri muda tu kutangazwa.

“Nimepokea majina mengine ya viongozi wa upinzani ambao wanataka kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wasaidizi wangu wameniambia yupo Mbunge mmoja anataka kurudi na ameniambia kuwa anataka kuja na madiwani saba kwenye jimbo lake, nasema hiki ni kimbunga na wataisoma namba kweli kweli.“amesema Rais Magufuli leo Desemba 18, 2017, kwenye Mkutano Mkuu wa 9 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao unafanyika mjini Dodoma.

Hata hivyo, Rais Magufuli amesema kuwa CCM wataendelea kupokea na kuwatangaza watu ambao wanahamia kwenye chama hicho na kudai kuwa lazima kwanza wajiridhishe ili wasije kupokea na watu wengine ambao hawana mpango mzuri kwa CCM.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger