Monday, December 18, 2017

Maleek Berry Atamani Kufanya Kolabo na Diamond.


Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Maleek Berry amesema anatamani kufanya kolabo na Diamond kutokana ni msanii mkubwa.

Muimbaji huyo katika mahojiano na The Playlist, Times Fm amesema ameiachia menejimenti yake kazi ya kumpata Diamond ili kufanikisha hilo ila endapo watashindwa atamtafuta mwenyewe.

“Natamani sana kufanya kolabo na Diamond ni mwanamuziki aliyekamilika ndio maana yupo juu, ana kila kitu”  alisema Maleek Berry.

Pia ameongeza kuwa msanii mwingine anayetamani kufanya naye kolabo ni pamoja na Vanessa Mdee na kueleza kuwa wamekuwa wakizungumza mara kwa mara.

Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger