Tuesday, December 19, 2017

Jakaya Kikwete: Eti Vyuma Vimekaza? Vumilieni tu

RAIS Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewataka watanzania kuwa wavumilivu kutokana na kauli zinazosemwa na vijana mitaani kuwa vyuma vimekaza wakimaanisha maisha yamekuwa magumu tofauti na kipindi cha nyuma.Kikwete amesema hayo jana Desemba 18, 2017 wakati akitoa salam kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM ambao umefanyika Dodoma ukiendana na uchaguzi mkuu wa chama hicho.“Hakuna kazi ngumu duniani kama urais, uzuri na ubaya wa kazi hii unakuwa mpweke, kila mmoja anakuletea shida zake wewe… Magufuli amefanikiwa kwa kiasi kikubwa ndani ya miaka miwili, inaleta matumaini kwa Taifa na kwa CCM.“Mambo ya kufanya katika nchi ni mengi, huwezi kuyamaliza yote ndani ya miaka miwili. Tunayasikia ‘oooh mara vyuma vimekaza’, kuweni na subira, viongozi wetu ni makini, wanayatambua matatizo yanayowakabiri wananchi wetu, wanayatafutia ufumbuzi,” alisema Kikwete. MTAZAME HAPA:
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger