Tuesday, December 19, 2017

Hebu Tuzungumzie Kidogo ishu ya Vanessa Mdee Kupata Dili Nono Ambalo Halijawahi Tokea Afrika

Nimekutana na taarifa 'njema' ambazo zinamhusisha msanii wetu pendwa, Vanessa Mdee ambaye alishawahi kuitwa Central na Makonda, kwamba amepata dili nono la kusaini na Lebo ya Kimataifa ya Muziki (Universal Music Group), akiwa ni msanii wa kwanza kutoka Afrika kupata dili hilo..

Mdee.JPG

Kwa lugha nyepesi, Vanessa amesainiwa na Lebo namba moja duniani ambayo inasimamia wanamuziki nyota na mahiri maarufu wakiwemo Jay Z, Elton John, Rihanna, Lady Gaga, Mariah Carey, Lil Wayne, Kanye West, Adele nna wengine wengi..

Yaani, hakuna msanii ambaye amewahi kusaini na lebo hiyo halafu asifanikiwe kukua kimuziki duniani. Hakuna.

Kwa ufupi, Vanessa anaenda kuwa kundi la wasanii namba 1 mashuhuri na tajiri duniani (A-List Artists)

Ifahamu hii lebo kwa undani Universal Music Group, the world's leading music company | Home Page - UMG

Mnasemaje Wadau?
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger