Wednesday, December 20, 2017

Faini Kutozwa kwa Watakaohubiri Kwenye Mabasi


Baraza la Ushauri wa watumiaji wa huduma za safiri wa nchi kavu na majini, SumatraCCC limekitaka chama cha wamiliki wa mabasi nchini TABOA na washirika wao kuhakikisha wanasimamia vyema suala la baadhi ya watu kugeuza na watu kuwa sehemu ya mahubiri suala mabalo limekuwa likilalamikiwa kila mara.

Akizungumza na waandishi na habari, Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri watumiaji Sumatra, Oscar Kikoyo, alisema kuwa mabasi yatakayo kiuka kanuni hiyo faini zinawanyemelea.

‘Tuna kanuni mpya za mwaka 2017 ya usafiri na hii kanuni ilipigiwa kelele sana, lakini kulingana na kanuni ya 27(b) kipengele cha 3 mabadi si sehemu ya gulio wala mabasi si msikiti wala makanisa kwenda kuhubiri dini kule ndani, kufanya biashara pamoja ni miziki na filamu ambazo azikidhi viwango na desturi za Kiafrika, kama kuna mabasi yanakiuka hii kanuni wajue hii faini inawanyemelea ,’ alisema Kikoyo.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger