Thursday, November 9, 2017

Haya Hapa Maajabu ya Tunda la Tende Katika Mwili wa Binadamu


AFYA: Tende ndio tunda pekee lenye kuupatia mwili vitu vinne kwa wakati mmoja, vitamini, protini, wanga na mafuta.
-
Zifuatazo ni baadhi ya faida za Tende; -

1- Kwa watu wenye matatizo ya tumbo, nicotinic inayopatikana kwenye Tende husaidia kurekebisha matatizo ya tumbo na huleta ahueni kwa watu wenye matatizo ya kupata choo.

2- Tende husaidia kuuimarisha moyo. Iloweke tende kwenye maji kwa usiku mmoja na asubuhi kunywa maji hayo pamoja na tende zilizolewekwa baada ya kuondoa mbegu, ukifanya hivyo mara mbili kwa wiki, moyo wako utakuwa imara.

3- Tende husaidia pia kwenye tendo la ndoa. Iloweke tende kwenye maziwa ya mbuzi usiku, asubuhi changanya maziwa hayo na asali kisha kunywa, njia hii husaidia kuongeza nguvu na stamina za kufanya mapenzi.

4- Utafiti umeonyesha kuwa tende husaidia kutanua misuli ya mji wa mimba wakati mwanamke anapokaribia kujifungua, hii husaidia kumfanya mwanamke asipoteze damu nyingi wakati wa kujifungua.

5- Wataalamu wa vyakula, wanazichukulia tende kama chakula bora kwa wanawake wanaonyonyesha kwani husaidia kuyapa maziwa virutubisho muhimu vinavyomfanya mtoto awe na afya njema.

6- Tende husaidia kupunguza kiwango cha kilevi (alcohol) kwenye damu. Maji ya kunywa ambayo tende imelowekwa ndani yake husaidia kuondoa haraka alcohol mwilini.

7 - Tende husaidia kuchelewesha dalili za uzee na pia husaidia kurekebisha ngozi na huondoa mabaka ya kuungua na jua.

8- Kutokana na madini ya chuma kwenye tende, watu wenye upungufu wa damu hupata ahueni.

9- Vitamin B1 na B2 vilivyopo kwenye tende husaidia kuyapa nguvu maini.

10- Tende pia huleta ahueni kwa watu wenye kikohozi na mafua.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger