Friday, October 20, 2017

Prezzo Adaiwa Kufulia...Kula Unga Yadaiwa Kuwa Chanzo

JACKSON Ngechu Makini ndilo jina lake halisi, lakini kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya Afrika Mashariki na Kati, wanamtambua zaidi kama C.M.B Prezzo (Cash Money Brother’s President). Mshikaji mmoja hivi, msanii maarufu kutoka Kenya.

Wakati Tanzania inachukuliwa kuwa ndiyo chimbuko kwenye mafanikio makubwa zaidi ya muziki wa kizazi kipya Ukanda wa Maziwa Makuu, nchini Kenya na Uganda, ndiko ambako wasanii wake wa muziki huo waliweza kujiingizia kipato kikubwa na kuonekana matajiri.

Ingawa Prezzo, ambaye alianza kufahamika nchini mwanzoni mwa miaka ya 2000, amewahi kukiri kurithi utajiri kutoka kwa wazazi wake, lakini muziki umeongeza thamani na umaarufu wake, kiasi cha kutajwa kuwa miongoni mwa wasanii waliokuwa matajiri katika eneo hili.

Amefanya kazi na wasanii wengi wa Tanzania na kipindi kile cha mwanzo, alishiriki pia hata baadhi ya matamasha makubwa ya muziki na hivyo kujizolea mashabiki wengi, sawa na Wakenya wenzake kama akina Wahu, Nyota Ndogo na Naazizi.

Licha ya uwezo wake katika muziki, pia Prezzo ni muigizaji mzuri wa filamu huko kwao kiasi cha kumfanya kuwa miongoni mwa wakali wa filamu wa nchi hiyo yenye utitiri wa wasanii wa fani mbalimbali kama filamu, muziki na vichekesho. Amefanya ngoma nyingi zilizojizolea umaarufu mkubwa ambazo mara nyingi alipopanda stejini, alienda sawa na mashabiki, kama vile vibao chake gumzo, Get Down Prezzo kuuza baadhi ya ‘nyororo’ zake shingoni!

Lakini kama nyati aliyejeruhiwa, rapa huyo ameibuka na kukanusha vikali madai hayo, akisema bado yupo fiti, na kwamba baada ya kurejea Kenya akitokea Bongo, ambako anadaiwa ndiko alishindwa kufanya ‘recording’ hiyo, aliongeza mikufu mingine ya bei mbaya katika shingo yake.

Sijakutana na Prezzo muda mrefu ingawa ninatambua kuwa ni mtu wa bata, mmoja kati ya wasanii ambao kula maisha ni sehemu ya ‘lifestyle’ yake.

Hata hivyo suala la yeye kula unga au ameishiwa, yanaweza yakawa ni maneno ya mitaani, lakini sisi Waswahili tuna msemo wetu ambao mara nyingi umetuthibitishia ukweli, kwamba lisemwalo lipo!

Kula unga kunaweza kusiwe kwa kiwango cha wale wadogo zangu katika stendi za daladala ambao unawaona kabisa kuzidiwa na kuishiwa kunaweza kusifanane na watu wa kawaida mtaani. Watu wanasema 50 Cent amefilisika, lakini ufilisikaji wake haumaanishi kuwa maisha yamempiga kwa kiwango cha kushindwa kula anachotaka, kuendesha ‘mkoko’ anaohitaji au hata vitu vingine vya kawaida.

Mwenendo wake katika maisha yake ya kila siku ndiyo unaozaa maneno haya mtaani, kwa sababu watu hawawezi kuzusha kitu ambacho hakiakisi matendo yake. Mbona hawamzushii Jaguar, Sauti Soul au Erick Omondi? Cha msingi ninadhani ni wakati wa Prezoo kujitazama upya katika kioo chake, kwa sababu kinachosemwa huku ni kivuli cha matendo yake. Anaweza kuwa anatumia unga na huenda akaunti yake ya benki imeanza kurudi nyuma vilevile, tuuache muda utamaliza kila kitu kwa kutuambia ukweli!

Kula unga, kuishiwa, muda utatuambiana Leo ni Leo aliomshirikisha T.I.D. Lakini bahati mbaya ujana una mambo mengi na hasa ukiwa katika nafasi nzuri kifedha kama ilivyo kwa Prezzo.

Ghafla zikaibuka tuhuma kuwa alikuwa anatumia madawa ya kulevya, kitu ambacho kimewaathiri vijana wengi wa Afrika Mashariki, hasa wasanii. Tuhuma hizi zimekuwa ni ngumu kuthibitika kwa sababu jambo hili hufanywa kwa siri, ingawa athari zake zinaanza kujitokeza baada ya muda, wakati mwingine kwa muonekano wa mtumiaji au matendo yake.

Wakati mmoja Prezzo aliwahi kumshika sehemu mbaya mtangazaji Betty Kyalo wa Kituo cha Televisheni KTN wakati akimfanyia mahojiano kitendo ambacho kilichukuliwa kuwa ni uzalilishaji. Mbali na hilo kilizua gumzo kubwa Afrika Mashariki, kiasi kilichosababisha mama mzazi wa msanii huyo kumuomba radhi mtangazaji huyo, huku hasimu wake mkubwa kimuziki, Jaguar akikebehi mtandaoni kuwa anamkaribisha ‘Rehab’.

Achana na hiyo, juzikati, watu wamemtuhumu kuwa licha ya kutajwa kuwa ana mkwanja mrefu, lakini hivi sasa amefulia, wakidai alishindwa kulipia hela ya kurekodia hadi kulazimika.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger