Saturday, October 28, 2017

Mbinu 10 za Kuoongeza Mbegu za Kiume (Sperm Count)

Mwanaume mwenye uwezo wa kuzalisha anahitaji kuwa na mbegu zisizopungua milioni 20, chochote chini ya hapa kinaweza kuwa sababu ya kutokutungisha ujauzito.

Ikitokea umegundulika kuwa na mbegu chache, ni nyepesi sana na hazina nguvu za kukimbia vya kutosha basi makala hii itakupa maelezo juu ya mbinu 10 zinazoweza kukusaidia kuongeza uwingi wa mbegu zako bila gharama yoyote.

Visababishi vya mbegu kuwa chache:

Kuna vitu vingi vinavyoweza kusababisha tatizo la mbegu chache na ugumba kwa ujumla kwa wanaume, kwa bahati nzuri vingi ya vitu hivyo tunao uwezo wa kuvidhibiti kwa kupunguza matumizi yake.

Vitu hivyo ni pamoja na:

• Vifaa vya kieletroniki – Tafiti zimeonyesha vifaa vingi vya kisasa vya kieletroniki vinasababisha kushuka kwa wingi na ubora wa mbegu kwa wanaume wengi miaka ya sasa kwani mionzi yake hupelekea joto lisilohitajika katika mifuko ya mbegu za kiume.

Vifaa hivi ni pamoja na simu na Kompyuta.

Unashauriwa kutokuweka simu ndani ya mfuko wako wa suruali kwa kipindi kirefu na kutokuweka kompyuta mpakato (laptop) kwenye mapaja yako wakati wote ukiitumia.

Ni mhimu pia kutokutumia masaa mengi kutwa nzima ukiwa kwenye kompyuta.

• Vifaa vya Intaneti visivyotumia waya – Siku hizi tofauti na zamani, kuna teknolojia mpya imeingia ya kuunganisha intaneti kwa kutumia vifaa visivyotumia waya (wireless internet) au kwa lugha nyepesi hujulikana kama Wi-Fi.

Vifaa hivi vinapunguza wingi wa mbegu, uwezo wa mbegu kukimbia na kuharibu muundo asili wa mbegu kwa ujumla (DNA fragmentation).

Wanaume wenye tatizo la uzazi wanashauriwa kutotumia aina hii ya vifaa vya kuunganishia intaneti kwenye kompyuta zao na vile vile kutokuweka simu kwenye mifuko yao ya mbele ya suruali.

• Uvutaji wa Sigara – Uvutaji sigara, bangi na bidhaa nyingine za tumbaku huharibu ubora wa mbegu za kiume.

Hilo halihitaji majadiliano. Habari njema ni kuwa madhara yaliyosababishwa na uvutaji sigara yanaweza kurekebishika ikiwa tu utaamua kuacha kuvuta.

Huhitaji dawa kuacha kuvuta sigara, unahitaji kuamua tu kwamba sasa basi na hakuna lisilowezekana kwa mtu mwenye maamuzi na mwenye ndoto za maisha mazuri ya kiafya.

Vingine vya kuviacha ni pamoja na bangi na madawa mengine yote ya kulevya.

• Viuavijasumu na homoni katika vyakula – Viuavijasumu (pesticides) vinavyotumika katika mazao mbalimbali mashambani miaka ya sasa ni sababu mojawapo ya tatizo la homoni kutokuwa sawa kwa wanaume wengi.

Kwenye bidhaa nyingi za maziwa za viwandani sasa huongezwa homoni kama vile homoni ya estrogeni ambazo hazihitajiki katika mwili wako.

Vyote hivi vina madhara katika afya ya mwanaume.

• Vyakula vyenye soya – Vyakula vyenye soya ndani yake hasa vile vya viwandani kama vile maziwa ya soya, burger za soya nk si vizuri kwa afya ya uzazi ya mwanaume.

Vinasemwa moja kwa moja kuathiri ubora wa homoni ya testosterone homoni mhimu sana kwa afya ya uzazi wa mwanaume
.
• Unywaji pombe – Katika moja ya utafiti kwa wanaume wenye mbegu zenye ubora wa chini, matumizi ya kupitiliza ya unywaji pombe yalionyesha kuhusika na kupungua kwa mbegu za kawaida yaani mbegu nzuri zinazofaa kwa ajili ya uzazi.

• Matumizi ya vifaa vya plastiki – Wakati kifaa cha plastiki kinapowekewa chakula cha moto hutoa kitu kijulikanacho kama ‘xenohormones’ ambacho huigiza kama ni ‘estrogen’ ndani ya mwili na hivyo kupelekea matatizo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanaume.

• Joto kupita kiasi (Hyperthermia) – Mifuko ya mbegu za uzazi ya mwanaume inahitaji joto la chini kidogo ya lile joto la mwili kwa ujumla ili mbegu zibaki na afya.

Inasemekana kuwa hii ndiyo moja ya sababu viungo vya uzazi vya mwanaume vipo karibu nje kabisa ya mwili wake.

Joto linajulikana wazi kuharibu ubora wa mbegu na hivyo itakuwa vizuri kuepuka mazingira ambayo yanaweza kusabbaisha joto la moja kwa moja kwenye viungo vya uzazi vya mwanaume ikiwemo kuepuka kuvaa nguo za ndani zinazobana sana.

• Mfadhaiko (Stress) – Mfadhaiko au stress inaweza kuleta majanga makubwa katika homoni na kupelekea kushuka kwa uzalishaji wa mbegu za kiume.

Stress inahusika sana na tatizo la ugumba kwa wanaume wengi, na moja ya sababu ya stress hii ni ile hamu yenyewe ya kuwa na mtoto inapokujia kila mara kichwani.

Vile vile kuna presha kutoka kwa wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwamba kwanini huzai.

Hivi vyote ukiviweka kichwani na kuviwaza kila mara ni rahisi kwako kupatwa na tatizo la kupungua kwa mbegu na uzazi kwa ujumla.

Kuwa na amani, mwamini Mungu kwamba siku yako ipo, just relax kila kitu kina muda wake.

• Aina ya chakula unachokula – Chanzo kingine cha kuwa na mbegu chache au zisizokuwa na afya ni kutokula chakula sahihi na cha kutosha kila siku.

Kwa afya bora kabisa ya uzazi mwanaume anahitaji vyakula vyenye madini ya zinki (zinc) kwa wingi, selenium, Vitamin E, folic acids, Vitamini B12, Vitamini C na vyakula mbalimbali vinavyoondoa sumu mwilini (antioxidants).

• Kujichua (punyeto) – Hili ni janga kubwa miongoni mwa wanaume wengi wengi karibu kote duniani. Tabia hii ukiianza huwa ni vigumu kuiacha na ni rahisi sana kugeuka kuwa teja wa punyeto.

Madhara makubwa ya kujichua ni pamoja na kupungua kwa kasi kwa uwingi wa mbegu kwa mwanaume pia nguvu zake kwa ujumla na hivyo kutokuwa na uwezo wa kumpa mwanamke ujauzito.

Vingine ni pamoja na kuendesha baiskeli masaa mengi, kukosa muda wa mazoezi ya viungo na kutoshiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu.

MBINU 10 ZA KUONGEZA WINGI WA MBEGU ZA KIUME (sperm count)

1. Kula lishe bora

Chakula unachokula kina mchango mkubwa katika kutibu tatizo hili. Vyakula vingi vya kisasa havina uwezo wa kuongeza uwingi wa mbegu.

Kama utarekebisha tu aina ya chakula unachokula kunaweza kupelekea kutibu tatizo lako.

Punguza matumizi ya sukari na vyakula vya ngano. Ongeza zaidi matunda, mboga za majani na mafuta yenye afya.

Hii inaweza kusaidia kutibu tatizo lako la kuwa na mbegu chache kwa haraka sana.

Endelea kusoma zaidi hii makala hapa chini.

2. Acha kutumia vinywaji au vyakula vyenye kaffeina

Kama una tatizo la kuwa na mbegu chache ni vizuri ukaacha kutumia vinywaji au vyakula vyote vyenye kaffeina kwanza.

Navyo ni pamoja na chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi zote, malta, redbull, chokoleti nk.

Hivi vitu vyenye kaffeina ni sababu ya kupungua kwa uwingi wa mbegu za kiume.

3. Tumia kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu ni maajabu ya Mungu mwenyewe. Kitunguu swaumu kina Selenium na pia kinaondoa sumu mwilini vitu viwili mhimu kwa ajili ya kuongeza spidi ya mbegu.

Kitunguu swaumu kina kitu kingine kiitwacho ‘Allicin’ ambacho huongeza msukumo wa damu kwenda kwenye uume.

Ongeza kitunguu swaumu kwenye chakula unachopika.

Pia unaweza kutafuna punje 2 au 3 kila unapoenda kulala au unaweza kukatakata hizo punje 3 vipande vidogo vido (chop) kisha unywe na maji.

Usizidishe zaidi ya punje 3 kwa siku.

4. Kula ndizi

Ndizi hazifanani tu na uume kama unavyoweza kuwaza bali pia ni chakula kizuri kwa ajili ya afya ya uume wako. Ndizi zina kimeng’enya kimoja adimu sana kijulikanacho kama ‘Bromeliad’ ambacho husaidia kuziweka sawa homoni zinazohusiana na tendo la ndoa.

Ndizi pia zina Magnesiamu, Vitamini B1 na Vitamini C, vitu ambavyo ni mhimu sana kwa ajili ya kutengeneza mbegu za kiume.

5. Kula mbegu za maboga

Mbegu za maboga zina kiasi kingi ccha madini ya Zinki ambayo ni mhimu katika kuundwa au kutengenezwa kwa mbegu za kiume na homoni ya testosterone.

Pia zina vitamini B, C, D, E, na K ambazo zote ni vitamini mhimu katika kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa na nguvu kwa ujumla.

Pia mbegu za maboga zina kalsiamu, potasiaumu, niacin na phosphorous.

6. Kula zaidi mboga za majani

Mama alikuwa sahihi kumbe ingawa nilikuwa nachukia nikikuta mboga majani badala ya nyama nikirudi kutoka shule.

Mboga za majani zinapunguza homoni ya ‘estrogen’ na hivyo kufanya homoni ya ‘testosterone’ ipatikane kwa wingi na kiurahisi zaidi na hivyo mbegu zako ziweze kuongezeka bila vipangamizi vyovyote.

7. Kunywa maji mengi kila siku

Hili ni suluhisho rahisi lisilohitaji gharama wala ugomvi wowote kukuelewesha. Mwenyewe unajua kuwa maji ni uhai na kuwa asilimia 75 ya mwili wako ni maji, sasa kama huna tabia ya kunywa maji ya kutosha kila siku sijuwi unategemea miujiza kutoka wapi.

Huhitaji kusikia kiu au mpaka upate hamu ya kunywa maji bali hili ni jambo la lazima kwamba huwezi kukaa bila kunywa maji halafu ubaki na afya bora.

Mbegu zako zimetengenezwa kwa maji, zipo kwenye hali ya kimiminika.

Kutokunywa maji ya kutosha kila siku kuna uhusiano wa moja kwa moja na kupungua kwa uwingi wa mbegu.

Kama utatekeleza mengine yote niliyoelekeza hapo juu halafu ukasahau kunywa maji hesabu umeshachemka tayari.

Kutegemea na uzito wako unaweza kuhitaji maji lita 2 mpaka 3 kila siku.

8. Tumia vyakula vyenye folic asidi kwa wingi

Katika utafiti mmoja wanaume walioongeza utumiaji wa folic asidi na zink waliongeza uwingi wa mbegu zao kwa zaidi ya asilimia 74 kwa muda wiki 2 tu.

Vyakula hivi ni pamoja na tunda la parachichi na karoti.

Hivyo isipite siku bila kula parachichi 1 kutafuna karoti moja kama una tatizo la mbegu chache.

Vingine ni pamoja na mbegu za maboga, ufuta, alizeti, maharage, chungwa, papai, bamia nk

9. Mayai

Mayai yanachukuliwa kama mbadala wa uhakika zaidi katika kuongeza uwingi wa mbegu pamoja na kuongeza spidi au kasi yake. Yana vitamini E nyingi na protini ya kutosha vitu viwili mhimu katika kuongeza mbegu.

Mayai yanafanya kazi nyingine mhimu nayo ni kuzilinda seli za mbegu za kiume kutoshambuliwa na vijidudu nyemelezi kirahisi ambavyo vinaweza kuwa sababu ya kupungua kwa mbegu zako.

Viinilishe vilivyomo kwenye mayai vinafanya kazi ya ziada ya kuzifanya mbegu zenye afya zaidi na zenye nguvu zaidi jambo ambalo ni mhimu kwa ajili ya uzazi kwa upande wa mwanaume.

Kumbuka ni mayai ya kuku wa kienyeji tu yanayofaa kwa kazi hii. Kila siku kula mayai mawili mpaka matatu kama una tatizo hili la kuwa na mbegu chache.

10. Spinach

Folic asidi ni kitu mhimu katika kuongezeka kwa mbegu za kiume. Spinachi na mboga nyingine za majani zenye rangi ya kijani ni mhimu kwa ajili hii sababu ya vitamini na kuweka sawa usawa wa ‘folate’ kwenye mfumo wako wa mwili.

Kama folate ipo chini kuna uwezekano ukawa unatengeneza mbegu zisizo na umbile linalotakiwa kwa uzazi na hiyo hupelekea shida na matatizo mengine ya uzazi upande wa mwanamke (birth defects) kama ujauzito kutoka mara tu mimba inapotungwa.
Share:
Weka Maoni yako Hapa

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger