Tuesday, March 20, 2018

Mpina Matatani kwa Kutohudhuria Mkutano wa Rais IKULU


Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina pamoja na Makatibu wao wameshindwa kuhudhuria mkutano wa 11 wa baraza la taifa la Biashara uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuendeshwa na Rais Dkt Magufuli.

Katika mkutano huo Rais Magufuli aliwahitaji mawaziri hao ili waweze kutoa ufafanuzi kuhusu maswala ambayo yameibuliwa na wafanyabiashara, lakini mawaziri hao pamoja na Makatibu wao hawakufika licha ya kuwa walialikwa na kupaswa kuwepo kwenye mkutano huo.

Kufuatia kutokuwepo kwa viongozi hao, Rais Magufuli alimuuliza Waziri Mkuu (Kassim Majaliwa) kama waliweza kuwaalika mawaziri hao na ndipo Waziri Mkuu alipojibu kuwa walipata mualiko na walipaswa kuwepo kwenye mkutano huo ingawa hakukuwa na taarifa yoyote ya wao kutokuwepo wala kutuma wawakilishi wao.

"Kwa hiyo wa Kilimo na Mifugo mawaziri na Makatibu wakuu wote hawapo?............Wao sio wajumbe wa mkutano huu? Alihoji Rais Magufuli ndipo Mawaziri Mkuu aliibuka na kutoa majibu kwa Rais Magufuli.

"Mawaziri wote wanaoguswa na sekta za uwekezaji na "kusupport" uchumi wetu wa viwanda, kilimo ni "facilitater" (msimamizi) wa viwanda na Mifugo naye pia ni wa viwanda walikuwa wapaswa kuwepo hapa kwa sababu walishapewa taarifa wote"
Share:

IGP Sirro, DCI na AG Mahakamani Kujibu Kesi ya Kumshikilia Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP) Abdul Nondo Kinyume na Sheria


Mahakama Kuu nchini  imetoa wito wa kuwaita DCI, IGP na AG kufika mahakamani siku ya Jumatano ya tarehe 21 kujibu kesi ya kutomfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi  (TSNP) Abdul Nondo.

Taarifa za wito huo zimetolewa na Wakili wa Mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Wakili Jebra Kambole.

Kambole amesema "Wito umetolewa  Mahakama kuu mbele ya Jaji Rehema Sameji. kwamba DCI, IGP na AG wanapaswa kufika mahakamani 21/03/2018 kujibu kesi ya Abdul Nondo".

Kambole amesema washitakiwa katika kesi hiyo itakayosikilizwa Jumatano ni ; IGP  Sirro ambaye ameitwa kwasababu yeye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini hivyo vituo vyote na polisi wapo chini yake lakini bado Nondo amekuwa hapatikani katika vituo vya polisi.

Aidha Kambole amesema kuwa katika jalada lililofunguliwa, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), naye kahusishwa kwa sababu mara ya mwisho Nondo alipokelewa na yeye alipofikishwa Dar es salaam kutoka Iringa na kwamba alimchukua kama muathirika wa tukio la utekwaji na siyo mshtakiwa.

Hata hivyo Kambole amesema ameshafanya jitihada nyingi za kutaka kuonana na mteja wake lakini hadi sasa juhudi zake hazijafua dafu.

Abdul Nondo anashikiliwa na jeshi la polisi tanguMachi 7, ambapo awali aliripotiwa kupotea kusikojulikana na kesho yake kujikuta Iringa, ambapo Kamanda wa Polisi  Kanda Maalumu, Lazaro Mambosasa amesema mpaka sasa wanamshikilia Nondo kwa ajilili ya upelelezi na watakapokamilisha watamfikisha mahakamani.
Share:

Waziri Mkuu Atoa Maagizo kwa Mawaziri Nchi 9 Kuhusu Magonjwa Yasiyoambukiza


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mapambano ya magonjwa yasiyoambukiza yatafanikiwa endapo sekta nyingine mbali na afya zitashirikishwa.

Majaliwa ameyazungumza hayo jana wakati akifungua mkutano wa 65 wa mawaziri wa afya wa Jumuiya za nchi za Mashariki, Kati na Kusini mwa bara la Afrika uliowashirikisha mawaziri kutoka nchi tisa.

Alisema kutokana na ongezeko la magonjwa hayo, nchi hizo zinapaswa kuangalia namna ambavyo zitatatua ongezeko hilo ili kupunguza gharama.

"Ili kuepuka  kutumia gharama kubwa katika kutibu magonjwa haya juhudi za makusudi zinapaswa kuchukuliwa ikiwemo kushirikisha sekta nyingine katika kutatua changamoto zilizopo lakini zaidi ni kuelimisha jamii kubadili mfumo wa maisha," alisema Majaliwa.

Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia (WB), Dk Paolo Belli alisema nchi hizo kwa sasa zinatakiwa kutumia teknolojia mpya ili kupata matokeo mapya katika magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa yasiyoambukiza, TB na vifo vya wajawazito na watoto.

Aidha, amezishauri nchi hizo kuangalia uwezekano wa kupunguza matumizi ya tumbaku kwa kuwa  yanasababisha madhara kwa watu wengi ikiwemo gharama za kutibu magonjwa mengi yatokanayo na madhara ya tumbaku.
Share:

Lowassa Ampa Tano Mkapa Kuhhusu Hoja ya Elimu.....Asema Ilikuwa ni Sera Yake na Ipo Katika Ilani yya CHADEMA


Waziri Mkuu za zamani, Edward Lowassa amemueleza Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kwamba kauli yake aliyoitoa juzi akitaka kuwepo kwa mjadala wa kitaifa kujadili hali ya elimu nchini ilikuwa ajenda yake tangu alipokuwa CCM.

Lowassa ametoa kauli hiyo jana Machi 19, 2018 katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa na msemaji wake, Aboubakar Liongo.

Katika taarifa hiyo, Lowassa ambaye alijiunga Chadema mwaka 2015 baada ya jina lake kukatwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM kusaka mgombea wake wa urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015, amesema suala la elimu pia lipo katika ilani ya uchaguzi ya Chadema.

Juzi jioni katika hafla ya kumuaga Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Profesa Idris Kikula, Mkapa alisema kuna janga katika elimu nchini na kushauri kuitishwa kwa mdahalo wa wazi utakaoshirikisha makundi yote ya jamii kwa ajili ya kujadili suala hilo.

Katika taarifa yake hiyo, Lowassa amesema amesoma na kusikia taarifa ya Mkapa akitaka kuwepo kwa mdahalo wa kitaifa kuhusu kushuka kwa elimu nchini.

“Nimefurahi kuwa Mkapa ameliibua suala hili kwani hiyo ilikuwa ni ajenda yangu ya kwanza tangu nikiwa ndani ya CCM na nje ya CCM. Pia Ilani ya uchaguzi ya Chadema, elimu ndio ilikuwa ajenda kuu na tulisema tutaita mjadala wa kitaifa kuhusu elimu na kuangalia wapi tumekwama na nini kifanyike,” amesema Lowassa.

Lowassa amedai ajenda hiyo sio ya CCM na hawataweza kuisimamia kwa sababu wanataka kuendelea kutawala,ila  hawataki Taifa lililoelimika vizuri na linaloweza kuhoji.
Share:

Ni Mwanzo Mpya....Habari Zilizoppo Katika Magazeti ya Leo Jumanne yya March 20


Share:

Monday, March 19, 2018

Wastara Aamua Kuwasaidia Wanawake Wenye Maisha MagumuMsanii wa Filamu nchini Wastara Juma, amesema kuwa ameamua kujitolea kusaidia wanawake wote wenye maisha magumu wakiwemo wanaoishi katika mazingira hatarishi, waliozalishwa na kutelekezwa na wenye matatizo mbalimbali.

Wastara ambaye ni balozi wa kusaidia wanawake nchini, ameshatembelea nchi mbalimbali ikiwemo Kongo na Burundi, kukusanya taarifa za wanawake wanaoishi kwenye mazingira magumu, amesema yeye kama mwanamke anaguswa na matatizo ya wanawake wenzake hivyo ana kila sababu ya kuwasaidia ili nao waishi katika maisha ya raha kama watu wengine.
Share:

Wema Sepetu: Mimi na Aunt Ezekieli Tunapendana Hakuna wa Kutugombanisha


MKALI wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu amelifungukia Ijumaa Wikienda kuwa, hakuna mtu wa kum-gombanisha na staa mwenzake, Aunt Ezekiel kwa kuwa wanapendana.

Katika mahojiano maalum na gazeti hili, Wema ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alitupia picha karibia kumi kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram akiwa na Aunt alisema kuwa, mara kwa mara wamekuwa wakigombana, lakini siyo kwamba hawapendani.

“Hakuna wa kunigombanisha na Aunt. Kama tunagombana, mtu wa pembeni anatakiwa kukaa kimya maana tukipatana mambo yanakuwa ni moto,” alisema Wema.
Share:

Uzuri Wangu Huwa Mademu Wakati Wote Wamenizunguka- Prezzo


Rapper kutoka nchini Kenya, Prezzo amejibu kuhusu tetesi za kuchana na aliyekuwa mpenzi wake Amber Lulu.

Prezzo ambaye kwa sasa yupo Tanzania kwa ajili ya promotion ya ngoma yake na Dogo Janja ameiambia FNL ya EATV kuwa kuachana kwao ni baada ya Amber Lulu kumuona na wanawake wengine bila kujua ukweli wa ukaribu wao ila bado anampenda.

“Uzuri wangu mimi huwa na mademu wakati wote wamenizunguka, shida nyingine mtu akiniona na demu fulani labda ni dada au binamu yangu kwa sababu mimi nina familia Tanzania tayari ni kosa,” amesema Prezzo.

Licha ya kauli hiyo ya Prezzo bado wawili hao wameonekena wakiwa pamoja kwenye mitandao ya kijamii, siku ya jana Amber Lulu katika ukurasa wake wa Instagram alipost picha wakiwa pamoja na kuandika; ‘Napenda nnyaa kama Mende ilo tendo tulitendee #hamsamia’.
Share:

Nisher Afunguka Matatizo Aliyopata Wakati Akiandaa WayuWayu na Dogo Janja


Mtayarishaji wa muziki wa BongoFleva nchini, Nisher Bybee amesema hakuna kikwazo chochote alichokipata wakati anaandaa video ya msanii Dogo Janja, 'Wayuwayu' na kudai pengine mke wake Irene Uwoya ndio aliyesababisha kuwepo hivyo.

Nisher ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha 'FRIDAY NIGHT LIVE' (FNL) inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya kuulizwa na swali na mtangazaji wa kipindi hicho kuwa ni tabu zipi alizipitia pindi alipokuwa anamuongoza Dogo Janja katika video ya wimbo huo ambayo amevaa uhusika wa mwanamke ambayo imekuwa gumzo mjini kwa jinsi rapa huyo alivyoabisha wana wa Arusha kwa mujibu wa maoni ya watu.

"Nilipigiwa simu na Madee kuwa anataka ku-shoot video mpya ya Dogo Janja lakini anataka aonekane yeye kama yeye, mimi nikaichukulia kama 'challenge' kwa kuwa sio kitu rahisi sana kukifanya lakini nikachukulia kama kazi na imekuja kutokea kitu kikubwa hata mwenyewe sikutegemea",amesema Nisher.

Pamoja na hayo, Nisher ameendelea kwa kusema "sasa sijui ni mke wake 'Irene Uwoya' ndio anamsababisha kuwa hivyo au vipi lakini Dogo Janja alikuwa anafanya vizuri kila 'shoot' tuliyokuwa tunafanya, hajanipa tatizo lolote la kurudia rudia ila kiukweli ni muigizaji mzuri wa pande zote"

Kwa upande mwingine, Nisher amesema licha ya kupewa lawama nyingi na baadhi ya watu ila anajivunia kuwepo kufanya kazi na Janjaro kwa kuwa amefanya ubunifu wa hali ya juu katika sanaa yake ya muziki kwa kuwa sio jambo rahisi kwa watu wengine kufanya hivyo.
Share:

Nikki wa Pili Atoa Ujumbe Mzito Kuhusu ViwandaMsanii Niki wa Pili ameitaka serikali inapotekeleza sera ya viwanda ihakikishe inajenga na kiwanda kila mkoa kwa ajili ya kutengeneza taulo za kike (pads), ili kuweza kuwasaidia watoto wa kike ambao hawana uwezo wa kumudu gharama za kununua.

Akiungana na East Africa Television, East Africa Radio na Msichana initiative, Nikki wa Pili amesema ni vyema kwenye kila viwanda 100 ambavyo vinatarajiwa kujengwa kwenye kila mkoa kama serikali inavyokusudia, ni vyema wakaweka kiwanda kimoja kwa ajili ya kutengeneza vitaulo vya kike.

“Kila mwezi binti anaenda kwenye siku zake, na tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 90 ya mabinti ambao wako sekondari hawana uwezo wa kununua pedi na kusababisha kukosa shule wakati wa kipindi cha mzunguko wa hedhi, jambo ambalo linampunguzia nguvu za kujiamini na kumuathiri kisaikolojia. Kuna kampeni ya kuhamasisha kujenga viwanda 100 kwa kila mkoa, kwa nini kwa kila viwanda mia tunavyotaka kujenga, tusijenge kiwanda kimoja tu cha kutengeneza pedi na kuwasaidia mabinti, hii itamsaidia kumjengea uwezo pia”, amesema Nikki wa Pili.

East Africa Television, East Africa Radio na Msichana Initiative, inaendesha kampeni ya #Namthamini kwa ajili ya kuchangisha pedi kwa ajili ya kuwasaidia wanafunbzi wa kike ambao hawana uwezo wa kununua bidhaa za kujisitiri wanapokuwa kwenye siku zao, ili waweze kubaki darasani na kuendelea na masomo bila kipingamizi chochote.

Share:

Rais Magufuli Aongoza Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara


Leo March 19, 2018 Moja ya shughuli inayoendelea ikulu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli Ambae ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara anaongoza Mkutano wa 11 wa baraza hilo.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ikulu, Gerson Msigwa kupitia ukurasa wa Twitter amesema kauli mbiu katika mkutano huo ni “Tanzania ya viwanda – ushiriki wa sekta binafsi”.

Share:

Baada ya Ua Jeusi la Zari, Wema Sepetu Penzi Lake Lachanua Upya Amtumia Ua Jekundu Diamond


Mapenzi ni kikohozi, hayawezi kufichika. Malkia wa filamu nchini Tanzania Wema Sepetu Jumatatu hii amepost picha ya ua la rose “Red Rose’ ambalo linadaiwa kuwa ni ishara ya upendo.

Mwigizaji huyo amekaa kimya kwa muda mrefu bila kuweka wazi mahusiano yake toka aachane na mchekeshaji Idris Sultan kitu ambacho siyo kawaida yake katika maisha yake.

Jumatatu hii amepost ua jekundu ikiwa ni ishara ya upendo huku akiandika ujumbe unaosomeka ‘A Red Rose is a Symbol of Love…’.

Hatua hiyo imechukuliwa tofauti na mashabiki wengi wa mrembo huyo baada ya hivi karibuni kuonekana kuwa karibu zaidi na mpenzi wake wa zamani, Diamond Platnumz.
Mashabiki hao wengi kupitia Instagram muda mchache baada ya mrembo kupost ua, amekuwa wakimtania kwa kusema kwamba huwenda mrembo huyo ameamua kurudia na Diamond ambaye ameachana na mama watoto wake, Zari The Boss Lady.

Maoni na mashabiki hao kupitia instagram.

udankimario

Madame wema nahisi kwa upande wa pili itakua ni Special kwa A boy From Tandale yan Simba😂😂

safiii_denis

Woyoooooooo kwetu raha siye twapost jekundu rose rose rose rose rose una rangi nyingi weweeeeee.

fatmarain39

Unahashuo wewe kwakuwa mwenzio kaweka black rose na wewe unatuekea red rose ovyoo

milly_ivan

Hatupendi black roses tunapenda red roses 😅😅😅 madam @wemasepetu

suleshcleverboytz

Jamanii Jamanii @wemasepetu kwan wamekukosea nini hawa watu @zarithebosslady@hamisamobetto @tundathebossbabemana huku Kunakoenda asaiv Vita Ya tatu Inaenda Kutokea SOOON 😂😂😂 

Bonyeza Play Hapa Chini Kuona Walichofanya Bilnass na Rosa Ree:
Share:

Amuuwa Mama Mkwe na Kumjeruhi Mkewe Kisa Unyumba


Kijana aliyefahamika kwa majina ya Joseph Medardi (32) mkazi wa Nyakahanga Wilaya ya Ngara mkoani Kagera amemuuwa mama mkwe wake Elizabeth Simon (70) kwa kumkata kata mapanga na kumjeruhi mkewe Elice Joseph (28) kisha na yeye kujimwagia petroleum.


Kijana huyo amefanya tukio hilo kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa na matatizo na mkewe kuhusu suala la unyumba jambo ambalo lilimpelekea kumrudisha mkewe huyo nyumbani kwa mama yake, ambapo amekaa huko takribani wiki tatu, siku moja kabla ya kikao cha kuwasuluhisha wanandoa hao ndipo kijana huyo ametekeleza mauaji hayo.

Mtoto wa marehemu Elizabeth Simon (70) ambaye ni Mchungaji Ezekia Simon amesimulia jambo hilo kwa undani zaidi na kusema kuwa chanzo cha yote hayo kuwa ni matatizo ya unyumba na kudai kuwa kijana huyo ambaye yeye ni shemeji yake alionekana amekuja na kusudio la kuwauwa wote yaani mama yake pamoja na mdogo wake huyo ambaye amejeruhiwa tu.

"Kisa cha kifo cha mama kimetokana na Mume wa dada kutoelewana katika habari za unyumba walikuwa na mgogoro kwa maana hiyo ikapelekea kumfukuza mkewe hivyo alikuja hapa yapata kama takribani wiki tatu yuko hapa nyumbani na baada ya hapo mimi kama Mkuu wa familia nilijaribu kutafuta njia ya kuwasuluhisha hivyo tarehe ambayo tulipanga kukutana ilikuwa jana ingawa hatukufanikiwa kukutana baada ya mzazi wa kijana kusema hakupata taarifa, matokeo yake yule kijana ndiyo amekuja akawashambulia mama pamoja na dada na kusababisha mauti ya mama"

"Yule kijana alikuja kwa lengo la kuuwa wale na yeye kujiuwa kwa sababu alipowashambulia na kuwajeruhi yeye alijimwagia Petroleum na kujichoma moto ndani ya nyumba hii hii"
Share:

Diamond Avunja Rekodi Nyingine Tena, Awapoteza Davido na Wizkid


Wazungu wanasema ‘Hard work Pays’ huu msemo unajidhihirisha kwa msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambaye kila kukicha anaendelea kuweka rekodi kwenye muziki wake na awamu hii sio views wa kwenye mtandao wa YouTube bali ni Subscribers.


Diamond kwenye akaunti yake ya YouTube tayari amefikisha Subscribers milioni 1+ na kuwa msanii wa Tatu barani Afrika kuwa na Subscribers zaidi ya milioni 1.

Kwa sasa Diamond Platnumz ameungana na wasanii kama Amr Diab kutoka Misri mwenye Subscribers milioni 1.6 na Saad Lamjarred kutoka Algeria ambaye ndiye anaongoza kwa bara la Afrika ana’Subscribers milioni 4.4 .


Kwa upande wa wasanii wengine kutoka Afrika kama Davido, Wizkid, Yemi Alade, Tiwa Savage, Sarkodie, Alikiba na Cassper Nyovest wote bado hawajafikisha Subscribers milioni 1 ingawaje hao wanatumia mtandao wa VEVO, na akaunti inayoongoza kuwa na Subscribers wengi ni ile ya kundi la PSquare ina subscribers laki 7.


Wiki iliyopita Diamond Platnumz aliachia album yake ya ‘A BOY FROM TANDALE’ na tayari imepokelewa vizuri na mashabiki wa muziki barani Afrika ambapo imeanza kutrend kwenye mitandao ya kununulia nyimbo kwenye baadhi ya nchi kama Burkina Faso.

Share:

Shindano la MO Margarine Star kutoa zawadi ya mil 4.2 kwa wanafunzi 10 nchini


Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) imeandaa shindano la kuimba wimbo wa MO Margarine kwa wanafunzi wa elimu ya msingi na sekondali, linalokwenda kwa jina la ‘MO Margarine Star’.

Akizungumza kuhusu shindano hilo, Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Group, Fatema Dewji ametoa masharti ya shindano hilo, kwamba kabla ya mwanafunzi kushiriki shindano hilo anatakiwa apate ridhaa kutoka kwa wazazi ama walezi wake.

Ameeleza kuwa, ili kushiriki shindano hilo, mwanafunzi anatakiwa ajirekodi video akiimba wimbo huo, na kuposti katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram au Facebook kisha kuishirikisha akaunti ya METL inayopatikana na kuweka hashtag ya #MoMargarineStar.

Dewji alisema zawadi kwa washindi ni Sh. 700,000 kwa mshindi wa kwanza, Sh. 600,000 kwa mshindi wa pili, Sh. 500,000 kwa mshindi wa tatu na kuanzia mshindi wa nne hadi 10 watapewa Sh. 400,000 kwa kila mmoja.

Share:

Taesa yatoa ufafanuzi jinsi ya kujisajili ajira 10,000 bomba la mafuta Hoima


Kufuatia Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi  “East Africa Crude Oil Pipeline (EACOP)”  kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani, Tanga nchini Tanzania, Taesa imetoa ufafanuzi namna ya kujisajili na ajira hiyo ili kuweza kutambulika.

Mradi huo ambao ujenzi wake unatarajiwa kuchukua kati ya miezi 24 hadi 36, unategemewa kuzalisha fursa za ajira takribani 10,000 wakati wa ujenzi na ajira zaidi ya 1,000 wakati wa uendeshaji wake.

Hivyo Watanzania wote wenye taaluma na ujuzi katika Sekta ya Mafuta na Gesi  wanatakiwa kujisajili TaESA kwa kuingiza taarifa zao lengo likiwa kuiwezesha Serikali kubaini idadi halisi ya Watanzania walio na sifa zinazohitajika na walio tayari kuajiriwa kwenye mradi huo.

Zoezi la usajili limekwishaanza na linatarajiwa kukamilika tarehe 30/03/2018, na usajili unafanyika kwa kujaza fomu maalumu inayopatikana katika tovuti ya www.taesa.go.tz, au kwa kufika kwenye ofisi zao za kanda zilizoko Dar es Salaam, Arusha, Dodoma na Mwanza.

Fomu zilizojazwa zinaweza kuwasilishwa kwenye ofisi zao za kanda au kwa barua pepe: eacop@taesa.go.tz. Kwa maelezo zaidi wasaliana nao kupitia namba zifuatazo: 0736 551 055; 0739 221 022; 0735 221 022; 0735 551 055 na 0282 541 840/1.

Mradi huu ni moja ya miradi mikubwa kutekelezwa nchini, unaotegemea kugharimu Dola za kimarekani 3.5 sawa na bilioni 8 za kitanzania

Bomba hilo litakuwa na urefu wa wa kilometa 1,445 ambapo ujenzi wa kilometa 1,115 za bomba hilo utafanyika nchini Tanzania.

Jumla ya wilaya 24 na vijiji 184 hapa nchini vinategemewa kupitiwa na bomba hilo katika mikoa 8 ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga.

Share:

Popular Posts

Copyright © MCHAMBUZI HURU | Powered by Blogger